Barua ya Dini Mbalimbali kwa Ajili ya Mustakabali Usio na Nishati Kisukuku
Kama viongozi wa dini na watu binafsi, tunawaomba viongozi wa dunia kuanzisha Mkataba wa Kuzuia Usambazaji wa Nishati kisukuku ambao:
Utaacha upanuzi wa uzalishaji mpya wa makaa ya mawe, mafuta, na gesi mara moja
Utaondoa taratibu uzalishaji uliopo wa nishati kisukuku kwa njia ya haki, huku mataifa tajiri yakiongoza mabadiliko haya
Utawezesha mpito wa haki kuelekea nishati jadidifu kwa wote, ukipa kipaumbele mahitaji ya jamii na wafanyakazi walioathirika