Linda Watu wenye Ualbino dhidi ya Saratani ya Ngozi: Wito kwa WHO kurejesha mafuta kinga ya jua kwenye Orodha ya Dawa Muhimu.

Nchi Wanachama wa Shirika la Afya Duniani (WHO)

Kujumuisha mafuta kinga ya jua (vizuia-jua ambavyo vinakidhi kigezo stahiki cha kiufundi cha ulinzi dhidi ya jua) kwenye orodha ya Shirika la Afya Duniani ya dawa muhimu itahakikisha kuwa yanapatikana kwa wingi zaidi na kwa bei nafuu.

Petition by
Africa Albinism Network
Dar es Salaam, Tanzania, United Republic of

To: Nchi Wanachama wa Shirika la Afya Duniani (WHO)
From: [Your Name]

Sisi, watu wenye ualbino, watu wenye ulemavu, na washirika wa harakati za ualbino;

Tunakusihi kurejesha tena vizuia jua (au mafuta kinga ya jua) katika Orodha rasmi ya WHO ya Dawa Muhimu na kuchangia mabadiliko ya muda mrefu kwa jamii ya Ualbino duniani kote.

Kwa nini? Kwa sababu saratani ya ngozi ndiyo muuaji namba moja watu wenye ualbino barani Afrika.

Kulingana na makadirio ya utafiti mmoja, karibu asilimia 90 ya watu wenye ualbino hupata au hufariki kutokana na saratani ya ngozi hadi kufikia umri wa miaka 40.

Hali ni mbaya zaidi kutokana na mabadiliko ya tabianchi. Kupanda kwa mionzi ya jua (ultraviolet (UV)) kunasababisha ongezeko la viwango vya saratani ya ngozi duniani kote, na watu wenye ualbino wakiwa katika hatari zaidi. Katika sehemu nyingi za Afrika, watu wenye ualbino wanakabiliwa na ugumu wa upatikanaji wa mafuta kinga ya jua kutokana na bei ghali na upatikanaji mdogo.

Tunachukua faragha yako kwa uzito. Hatutauza au kubadilisha maelezo yako. Gundua jinsi tunavyolinda na kutumia data yako binafsi katika Sera yetu ya Faragha.