Amani na Haki ya Mazingira Bora Sasa
Wanasiasa wote, ndani, kikanda, kitaifa na kimataifa
Vijana, mashirika ya kijamii, na watetezi wa mazingira ombi hili ni letu sote. Pakua hapa karatasi ya kukusanyia saini (https://actionnetwork.org/user_files/user_files/000/127/744/original/share-swahili-peace-and-climate-v2docx.pdf), ujaribu kujaza kwa marafiki, familia, au kikundi chako kisha upakie kwenye tovuti uliyotembelea hivi punde. Waite wengine wanaojali mazingira kuungana nasi. Harakati hii ni ya kizazi hiki na vizazi vijavyo.
Download the paper petition to gather signatures, press pdf here. Signatures can then be uploaded here on the right. Please use English. ________________________________________________________________________________________________________
Amani na Haki ya Mazingira Bora Sasa
Jiunge nasi katika kujenga harakati ya kudumisha amani duniani na kulinda mazingira yetu. Sasa ni wakati wa kushirikiana katika jamii, taifa na kimataifa kwa mazungumzo ya amani na kusitisha vita ili kutafuta suluhisho la kweli kwa changamoto za mabadiliko ya tabianchi na usimamizi wa rasilimali kwa haki.
Silaha na vita zinatumia mali nyingi ambazo zinahitajika kwa kutatua matatizo kama mabadiliko ya tabianchi, uhaba wa maji, na ukame. Uharibifu wa mazingira unaoletwa na vita kupitia mabomu, uchimbaji kupita kiasi na uchafuzi unasababisha athari mbaya kwa binadamu na mazingira.
Hatuwezi kuendelea kuishi kana kwamba tuna dunia nyingine. Tunahitaji kupunguza matumizi ya nishati kwa kutumia teknolojia safi na kuendeleza maisha ya kuhifadhi rasilimali. Jamii zinahitaji mabadiliko makubwa ya kijamii na kiuchumi ili kuhakikisha maendeleo endelevu kwa watu wa vijijini na mijini, hasa wanaofanya kazi katika kilimo, misitu, viwanda na huduma.
Vita husababisha maumivu watu huuliwa, kujeruhiwa, na kulazimika kukimbia makazi yao. Huduma za kijamii na miundombinu huharibiwa. Badala ya kugawanyika, tunahitaji kushirikiana kujenga amani ya kudumu.
Chama cha Amani Stockholm – Kikundi kazi kwa ajili ya Amani na Tabianchi
Marafiki wa Mazingira Sweden – Kamati ya Amani
Wasanii kwa ajili ya AmaniFridays for Future
Sponsored by
To:
Wanasiasa wote, ndani, kikanda, kitaifa na kimataifa
From:
[Your Name]
Tunawaalika watu binafsi na mashirika kushirikiana nasi kuunda kampeni ya pamoja kwa ajili ya amani, haki na mazingira bora. Tujenge mshikamano wa kimataifa wa kushughulikia athari za mabadiliko ya tabianchi. Tuwekeze kwenye chakula, elimu, afya na huduma za jamii badala ya silaha.
Tunaomba
--Amani na Haki ya Mazingira Bora Sasa
--Tupinge vita – kwa ajili ya mazingira na ustawi wa wote!
--Kwa dunia ya haki na matumaini!